Bima ya Elimu

Wajibu unaotekelezwa na Bima ya Elimu

Elimu ni moja katika ya urithi muhimu mzazi anaweza kumpa mtoto wake. Bima ya elimu inatekeleza wajibu muhimu kwa kulipa karo za shule ya mtoto. Hii ni kwa sababu ni wajibu wa wazazi kumsomesha mtoto wake.  Bima ya elimu huwawezesha wazazi kulipia karo za shule kuanzia sekondari hadi vyuoni. Hii ni kulingana na aina ya bima unayolipia. Unashauriwa kupangia bima hizo mtoto akiwa mdogo ili bima imsaidie akiwa anaingia shule ya sekondari.

Manufaa ya bima ya elimu

 1. Iwapo mnunuzi wa bima ya elimu ataaga dunia ghafla, gharama ya malipo ya bima hiyo itasimamishwa papo hapo. Iwapo jamaa ya aliyeaga itajulisha kampuni hiyo haraka iwezekanavyo na kuwasilisha stakabadhi zifaazo.
 • Kufuatia kifo cha mnunuzi, bima hiyo itaendelea bila garama ya malipo hadi kipindi ambapo bima hiyo ilikusudiwa kuanza kulipa malipo ya karo. Bima hiyo itaendelea kumlipia mtoto karo kana kwamba mzazi angali hai.
 • Fidia ya bima ya elimu haitozwi ushuru na serkali. Hii inamaanisha kwamba jumla ya fidia utakazolipwa kufuatia kukamilika kwa kipindi cha bima hazitatozwa ushuru.
 • Kuna aina nyingi za bima za elimu. Aina zingine zinaweza kulipia matibabu ya mtoto atakapolazwa hospitalini au kuhusika katika ajali na pia kugharamia mazishi ya mtoto ikiwa ataaga kabla ya kukamilika kwa kipindi cha bima.

Mambo Muhimu ya kuzingatia ukinuia kununua bima ya elimu

 1. Chukua bima ya elimu mapema katika maisha ya mtoto ili ulipe malipo ya chini.
 • Chukua bima ambayo una uwezo wa kugharamia hadi kukamilika kwa kipindi chake ili uepuke na kuisalimisha kisha kupoteza hela zako.
 • Iwapo mtoto uliyemchukulia bima ataaga dunai kabla ya bima kuanza kulipa, unaweza kubadilisha bima hiyo kwa mtoto mwingine wa miaka sambamaba ama miaka ya chini. Ni sharti ushauriane na kampuni ya bima kabla ya kuchukua hatua hiyo.
 • Nunua bima kutoka kampuni zilizodhinishwa na IRA pekee.
 • Pata ushauri kuhusiana na bima kutoka kwa kampuni ya bima, ajenti au broka wa bima au kutoka kwa IRA.
 • Hakikisha kwamba umepewa cheti (policy) cha bima na kampuni yako.
 • Hakikisha kulipia bima kikamilifu katika kipindi kizima.

Panapopatikana bima za elimu

Kuna kampuni nyingi za kuuza bidhaa za bima ya elimu. Kampuni hizi huuza bidhaa mbalimbali kupitia maajenti au mabroka. Pia unaweza kununua bima moja kwa moja kupitia kampuni ya bima.

Basi, kuwa huru kununua bima ya elimu ili ujihakikishie utulivu na amani wakati unapopatikana na tukio!

Halmashauri ya Kudhibiti Bima (IRA)

IRA ilibuniwa na serikali mnamo mwaka wa 2006 kwa jukumu la kuweka maangalizi, kudhibiti sekta ya bima, kusimamia na pia kuhakikisha kwamba yeyote anayehusika na biashara za bima anatekeleza kazi yake kwa njia za usawa na pia kutilia maanani manufaa ya wanunuzi bima. Jukumu kuu la IRA ni kuwalinda wanunuzi wa bima na jamii kwa jumla. Nia ya IRA ni kuhakikisha kuwa wanunuzi hao wanapata huduma wanaozilipia. IRA si kampuni ya bima  na hivyo haiuzi bima. IRA inawajibika kuhakikisha kuwa kampuni za bima zinashughulikia ipasavyo malalamishi yanayohusiana na bidhaa wanazouza. IRA huhakikisha kwamba ni malalamishi ya kweli pekee yanayoshughulikiwa bila kucheleweshwa. IRA pia inawajibika kuhakikisha kuwa wanunuzi bima wananunua kwenye kampuni zilizoidhinishwa na halmashauri hiyo wakiwemo maajenti na mabroka.

Huduma za IRA katika kusimamia maslahi ya Wakenya katika sekta ya bima ni za bila malipo. Unaweza kuelekeza suala lolote linalohusu bima kwa IRA ukitumia njia za mawasiliano zilizoorodheshwa nyuma ya brosha hii. 

Anwani za IRA

S.L.P. 43505 – 00100 NAIROBI

Zep- Re Place Off Mara Road – Upper Hill, Nairobi

Simu:(254)- 020- 4996000, 0727 563110

Simu bila malipo – 0800724499

Kipepesi: (254)- 020 – 2710126

Baruapepe: commins@ira.go.ke

Tovuti: www.ira.go.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *